Wamiliki wa ZE UTAMU Wasakwa na Jeshi la Polisi

JESHI la Polisi nchini linawasaka wamiliki wa mtandao unaojulikana kama ZE UTAMU ambao unakwenda kinyume na maadili za Kitanzania.
Jeshi hilo limetowa tamko kuwa wapo kwenye mikakati mikali ya kubaini wamiliki na wanaoendesha mtandao huo kwa nia ya kuwatia hatiani kwa kile kinachodaiwa kuwa wanadhalilisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa nchi.

Msemaji wa jeshi hilo amesema kuwa kutokana na vitendo vinavyofanywa na wamiliki wa mtandao huo Jeshi hili halitavumilia na limeamua kuwasaka moja kwa moja watu hao.

Amesema kuwa mtandao huo umekuwa ukitumia nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kutoa picha mbalimbali za kudhalilisha na za ngono ikiwemo na kukashifu viongozi.

Amesema kuanzia jana Maofisa wa Polisi ikiwemo na Tume ya Uchunguzi wa Mawisiliano wanakutana kwa kujadili kwa kina suala hilo ikiwemo na kubaini wamiliki.

Amesema hatua iliyofikia ya mtandao huo kudhalilisha wananchi pia na kutotoa maadili mazuri kwa jamii vitendo hivyo havitavumiliwa na Jeshi hilo.

Pia baadhi ya wananchi waliyohojiwa na NIFAHAMISHE walisema kuwa hatua iliyochukuliwa na JEshi la Polisi ni la msingi kwa kuwa Mtandao huo ulikuwa unaweka picha za kipuuzi na fedheha kwa umma wa Watanzania.

“Tunaomba wasakwe haraka iwezekanavyo ili mkondo wa sheria ushike mahali pake kwa kuwakamata wote wanaojihusisha na mtandao huo”.



2 comments:
Anonymous said...
 

Haikuwa blog mbaya, Kama inavyosemwa

Anonymous said...
 

Ilifundisha watu adabu, hasa viongozi Ambao wameoza kitabia.

Post a Comment

Copyright © 2009 Bloggerized by : CTU | Inspired By ReedzSolution : ReedzSolution