Baada ya DECI: Upatu mwingine uitwao Masebe wanaswa

Siku chache tu baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutoa agizo la kufuatiliwa kwa taasisi nyingine za upatu haramu wa aina ya DECI ambao huwezesha watu kupanda na kuvuna mapesa kwa faida nono, hatimaye Jeshi la Polisi Jijini Dar limefanya kweli na kuinasa taasisi nyingine ya aina hiyo iitwayo Masebe Business Group.

Kwa mujibu wa taarifa za Kipolisi, taasisi hiyo iko pale Buguruni Jijini na kwamba hadi sasa, ina wanachama kibao ambao wamepanda mapesa yao kwa matarajio ya kuyavuna kwa faida nono.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova, amesema polisi wanaendelea na msako mkali dhidi ya taasisi za aina hiyo kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu Pinda wakati.....

Kwa Habari Zaidi Nenda Hapa.



0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2009 Bloggerized by : CTU | Inspired By ReedzSolution : ReedzSolution